Habari

GEITA: Mama amcharanga mapanga mwanae wa kumzaa kisha amchemsha supu viungo vyake

Mwanamke mmoja mkoani Geita amekamatwa na Jeshi la Polisi mkoani humo kwa tuhuma za kumuua mtoto wake wa kumzaa kwa kumkatakata na panga kisha kuchemsha vipande vya mwili wa mtoto huyo kwa lengo la kunywa supu.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo, Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani Geita, Dismas Kissusi amesema tukio hilo limetokea Juni 21, 2019 katika Kijiji cha Buligi, Kata ya Senga wilayani Geita.

Jeshi la polisi limemtaja mwanamke huyo kuwa ni Happyness Shedrack (36) na historia yake ya nyuma inaonesha kuwa ana matatizo ya akili, Mtoto huyo aliyeuawa ana mwaka mmoja.

Hata hivyo upepelezi bado unaendelea na Jeshi la Polisi limedai ukikamilika atapelekwa mahakamani kwa tuhuma za mauji.

Chanzo: https://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa/Mama-afanya-mauaji-ya-kikatili-kwa-mwanawe–/1597296-5168186-5sj9f5z/index.html

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents