Burudani

Beef ya Cassidy vs Meek Mill: Mwana FA, Godzilla na Chidi Benz wako upande gani?

meek vs cass

Beef kati ya rappers wa Philadelphia, Pennsylvania, nchini Marekani Robert Williams aka Meek Mill na Barry Adrian Reese aka Cassidy imezidi kupamba moto baada ya Cassidy kuachia diss track yenye dakika 10 iitwayo Raid.

Beef hiyo imevuta hisia si za wamarekani tu bali hata wasanii wakubwa wa Hip Hop Tanzania wanaifutialia kwa kwa karibu. Hata hivyo wengi wao wanaonekana kuwa upande wa Cassidy zaidi.

Kupitia Twitter Chidi Benz ameandika, “Namkubali Cassidy,mtulivu na anajua kusema.”

Naye Godzilla ameikejeli tweet ya Meek Mill aliyoandika, “Now they re-signed him back that’s crazy,” kwa kumwambia kwa Kiswahili, “Nenda kajibu studio acha mbwembwe.”

Kuhusu uwezekano wa Meek Mill kuijibu Raid Mwana FA ameandika, “kakaa,utajibu nini mle.”

Nani atashinda? Meek Mill ama Cassidy?

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents