Bongo5 ExclusivesBurudaniHabariMuziki

Tundaman aacha EP yake ya ‘2022 EP’ rasmi

Nyota wa Muziki wa Bongo Fleva, Khalid Ramadhan Tunda al-maarufu ‘Tundaman’ ameachia rasmi EP yake aliyoipa jina la ‘2022 EP’ kupitia App namba moja Afrika, Boomplay.

Akizungumza kuhusu EP hiyo, Tundaman amesema “2022 EP” imeandaliwa na watayarishaji mahiri wa muziki wa Bongo fleva ambao ni; – T-Touch, Mafia, Mesen Selekta na Shirko. EP imebeba mikwaju ya moto saba; – Badman ft Harmonize, Nimeshindwa ft Darassa, Kizaa zaa ft Alikiba, Mchawi Ndugu ft Chid Benz, Vita ni vita ft Nay wa Mitego, Nipe ripoti II ft Spack na Sawa ambayo niko peke yangu.

 

Hii ni comeback yangu kwenye gemu ya muziki wa Bongo fleva kwa kuwa nimekuwa kimya kidogo na ili kuwafurahisha mashabiki nimeona niwape zawadi ya mikwaju saba ya moto. Vilevile, nimeona niiachie kupitia Boomplay kwa kuwa ni jukwaa namba moja la muziki barani Afrika hivyo nina uhakika wa kazi yangu kusikilizwa na watu wengi zaidi”.

Ili kuipa nguvu EP hiyo, Tundaman amejipanga kufanya ‘media tour’ na ‘promo’ mbalimbali katika kuhakikisha EP hiyo inaenda mjini.

Tundaman ni moja ya wasanii nguli kwenye gemu ya Bongo fleva ambae ametamba na vibao kadhaa ambavyo vimemletea sifa na umaarufu mkubwa ndani na nje ya Tanzania.

Mpaka sasa mkali huyo wa Bongo fleva anaendelea kutamba na kibao chake cha Badman alichomshirikisha Harmonize. Kibao hicho kimeendelea kuvunja rekodi mbalimbali na mpaka sasa kina jumla ya wasikilizaji zaidi ya milioni 2, Boomplay.

Unaweza kuisikiliza na kupakua albamu ya Tundaman bure kupitia linki ya Boomplay hapa:- https://www.boomplay.com/albums/50926884?from=home

Boomplay ni App inayoongoza kwa huduma ya kupakua na kusikiliza muziki inayotolewa na Kampuni ya Transsnet Music Limited. Jukwaa la Boomplay linajumuisha mamilioni ya nyimbo, video na habari za burudani ambalo huwawezesha watumiaji wake kusikiliza na kupakua nyimbo na video wanazozipenda kila siku, wiki hadi mwezi huku ikiwezesha kufikia vipengele vinavyolipiwa kama vile usikilizaji bila matangazo na kuhifadhi muziki kwa ajili ya kusikiliza pale unapokua huna bando. Kwa sasa Boomplay ina zaidi ya watumiaji milioni 75 wa kila mwezi (MAU) na orodha ya nyimbo zaidi ya milioni 80.

Huduma hii inapatikana duniani kote kwenye simu kupitia Google Play Store ya Android, App Store ya iOS na kwenye wavuti kupitia www.boomplay.com. Kampuni hiyo ina ofisi za kanda nchini Tanzania, Nigeria, Ghana, Kenya, Cote d’Ivoire na Cameroon.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents