Burudani

Waziri Mchengerwa kupokea taarifa ya kamati ya namna ya ugawaji wa Mirahaba

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Mohamed Omary Mchengerwa leo Agosti 12, 2022, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye hafla ya kupokea taarifa rasmi ya namna bora ya ya kusimamia HAKIMILIKI na Ugawaji wa Mirahaba kwa wasanii nchini kutoka kwa Kamati aliyoiteua Julai Mosi mwaka huu katika Ukumbi wa Kimataifa ya Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere kuanzia saa 11 jioni jijini Dar es Salaam.

Uteuzi wa Kamati hiyo, ulitokana na malalamiko ya wadau hususan wa Sekta ya Sanaa nchini kuhusiana na namna mirabaha inavyokusanywa na kugawanywa, kuwepo kwa vitendo vya uharamia katika kazi zao na elimu duni kwa wadau kuhusu masuala hayo.

Aidha, uundaji wa Kamati hiyo ulitokana na maelekezo ya Mhe. Rais ya kuitaka Wizara kusimamia na kutafuta muarobaini wa changamoto za mirabaha kwa wasanii aliyoitoa Mei 30, 2022 jijini Dar es Salaam.

Pia, Mhe. Mchengerwa anatarajia kuwakaribisha nyumbani na kuwapongeza wachezaji mashujaa walioweza kurejea na medali kutoka kwenye Mashindano ya Jumuiya ya Madola yaliyomalizika hivi karibuni Birmingham nchini Uingereza

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents