Picha: Vodacom yawatangaza washindi 35 wa droo ya miito ya simu
Kampuni ya huduma ya simu za mkononi nchini, Vodacom, leo imekutana na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, kuwatangaza washindi 35 wa droo ya miito ya simu iliyozinduliwa na kampuni ya Vodacom wiki iliyopita. Kupitia droo hio, wateja watano wanajishindia shilingi 50,000 kila siku.
Meneja Huduma za Ziada wa Vodacom Tanzania, Matthew Kampambe (katikati) akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuwatangaza washindi 35 wa droo ya miito ya simu iliyozinduliwa na kampuni ya Vodacom wiki iliyopita. Kupitia droo hiyo, wateja watano wanajishindia shilingi 50,000 kila siku. Kulia ni Bw. Salum Mwalimu, Meneja Mahusiano ya Nje wa Vodacom na kushoto ni Mw. Mrisho Millao, Ofisa wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha
Meneja Huduma za Ziada wa Vodacom Tanzania, Bw. Matthew Kampambe, akizungumza na mmoja wa washindi wa shilingi 50,000 kwenye simu wakati akichezesha droo ya miito ya simu iliyozinduliwa na kampuni ya Vodacom wiki iliyopita.