Michezo

Donald Sterling apinga Clippers kuuzwa kwa gharama ya dola bilioni 2

Mkurugenzi wa zamani wa Microsoft, Steve Ballmer, amefikia makubaliano na timu mashuhuri ya mpira wa vikapu ya Los Angeles Clippers ya kuinunua timu hiyo kwa dola bilioni mbili.

Donald Sterling

Hata hivyo ununuzi huo unapingwa na mmiliki wa sasa Donald Sterling. Mpira wa vikapu ni maarufu sana Marekani. Na kwa sababu hushirikisha wachezaji wengi weusi matamshi ya Sterling yalihofiwa yangevuruga biashara ziinazotangazwa kupitia mchezo huo.

Sterling alitozwa faini ya £1.5m na pia amepigwa marufuku kuhusika kabisa na mchezo huo baada ya kashfa mliomkabili pale ilipoonekana kanda aliyorekodiwa akitoa matamshi ya ubaguzi wa rangi kuhusu wachezaji weusi wa mpira huo wa vikapu uliomaarufu sana Marekani.

Katika kushindania ununuzi huo, Ballmer aliwapiku wakinzani wake wawili akiwemo magwiji mahiri katika sekta ya vyombo vya habari akiwemo David Geffen na Oprah Winfrey. Ballmer alistaafu kutoka Microsoft miezi mitatu iliyopita lakini bado ana kima kikubwa cha hisa katka kampuni hiyo zilizo na thamani ya zaidi ya dola billioni kumi na tatu.

Source:BBC

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents