Burudani

Abdu Kiba adai hakuna staa wa kike Bongo anayefaa kuolewa na Alikiba

Msanii wa Bongo Fleva, Abdu Kiba amedai hukuna staa wa kike Bongo mwenye vigezo vya kuolewa na Alikiba ambaye ni kaka yake.

Muimbaji huyo amesema ingawa Alikiba ni mtu wa kawaida ila anahitaji mwanamke wa aina yake na mwenye kushika sana dini.

“Sijamuona bado staa huyo wa kike ambaye nitasikia Alikiba anatoka nae halafu nikafurahi, bado sijumona wa kuweza kumfaa Alikiba kwa sababu ninawaona. Hawana kasoro ni wasichana wazuri na warembo ila bado hawajafikia hatua ya wao kuwa na mtu kama Alikiba,” ameiambia XXL ya Clouds FM.

“Alikiba ni mtu wa kawaida kwanza, na ni mtu mwenye busara mpenda amani, mpenda ucheshi, kwa hiyo anahitaji mtu ambaye ameivaa sana dini,” amesisitiza.

By Peter Akaro

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents