Burudani

Abdu Kiba aeleza sababu za ukimya wa kundi lao la Kiba Square na mipango yao mipya

Msanii wa muziki Abdu Kiba amesema ukimya wa kundi walilolianzisha yeye na kaka yake Alikiba, Kiba Square ulitokana na kumpa nafasi kaka yake kufanya ‘comeback’.

kiba

Kiba Square ni kundi la wasanii wawili ndugu, Alikiba na Abdu Kiba, kama ilivyo kwa kundi la mapacha wa Nigeria P-Square.

Abdu ambaye wiki tuliyoimaliza ameshoot video ya wimbo wake mpya aliomshirikisha Ruby ’Ayaya’, amesema project za Kiba Square zitaanza kusikika tena baada ya video ya kaka yake na yake kutoka.

“Kiba Square ipo ila kutokana na gap ambalo niliweza kumuachia bro kwa muda mwingi ambao yeye amekuwa kimya, na kuomba nafasi ya kurudi kuja ku kufuta vumbi kiti chake ndio sababu ilionekana kwamba Kiba Square imenyamaza. Ila Kiba Square ipo na project zinaendelea nadhani baada ya mimi kutoa huu wimbo (Ayaya) nikimaliza kushoot nadhani zitagongana video mbili kwa wakati mmoja video ya ‘Ayaya’ na Chekecha halafu tunasimamisha project ya Kiba Square kwasababu kila kitu kipo tayari ni nprogram ndio ambazo zinapishana tu”. Alisema Abdu Kiba alipohojiwa na Millard Ayo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents