Michezo

Achana na Champions League na Europa League, UEFA yaongeza mashindano mengine makubwa, fursa kwa ligi ya Samatta

Shirikisho la soka barani Ulaya, UEFA limetangaza rasmi mashindano mengine mapya ambayo yatafanya kuwa na jumla ya michuano mitatu baada ya miwili iliyokuwa nayo kwa sasa ambayoni UEFA Champions League na Europa League.

p1dli85a9d7d34gp191chu21ka39.jpg

Katika kikao chake kilichofanyika nchini Slovenia shirikisho hilo limeadhimia kuanzisha michuano hiyo mipya itakayo julikana kama UEFA Europa Conference League ambapo imepangwa kuanza kutimuavumbi msimu wa 2021.

Michuano ya UEFA Europa Conference League ni michuano mipya ambayo imeanzishwa kwa lengo la kuzipa nafasi klabu zinazotoka nchini wanachama wa UEFA ambazo zinapatikana chini ya viwango vya juu kupata nafasi zaidi ya kushiriki micbuano ya Ulaya.

Michuano hii itakuwa ikichezwa siku ya alhamisi kama kawaida na itakuja na mabadiliko kidogo ambapo itapunguza klabu zinazoshiriki michuano ya Europa League ambazo kwasasa ni klabu 64 lakini zitapungua mpaka kufikia klabu 32 kwenye michuano ya Europa League.

Kisha timu hizo zitakazopunguzwa zitaenda kushiriki michuano hiyo mipya ambayo imeandaliwa kama michuano mitatu midogo nyuma ya UEFA Champions League na nyuma ya Europa League.

Hivyo ligi zote tatu zitakuwa na timu 32 uku zikitengeneza makundi 8 uku kila kundi kukiwa na timu 4.

Mshindi wa michuano ya Europa League atafanikiwa kufuzu kama kawaida kucheza michuano ya UEFA Champions League kwa msimu ujao na yule bingwa wa michuano hii mipya (UEFA Europa Conference League) pia atapanda na kucheza michuano ya Europa League kwa msimu ujao.

Hivyo ligi hii mpya imeanzishwa ili kuzipa nafasi timu zinazopatikana kwenye nchi zilizo chini ya viwango vya UEFA ambazo zinatoa mshiriki mmoja tu kucheza michuano ya juu.

Mfano klabu ya KRC Genk anayochezea Mtanzania Mbwana Samatta wameshiriki michuano ya UEFA Champions League kwa msimu huu kwa vile timu yao ilikuwa bingwa wa ligi msimu uliopita hivyo nchi ya Ubelgiji imetoa mshiriki mmoja tu jambo ambalo ni tofauti kwa nchi kama Uingereza ambayo ina timu 4 zinazoshiriki michuano hii.

Image result for Samatta and UEFA

Sasa michuano hiyo mipya itakavyoanza itatoa fursa kwa timu nyingi kutoka nchi kama Ubelgiji ambapo anachezea Samatta, Uholanzi, Uturuki na nyengine zitakuwa zina toka timu nyingi zaidi zitakazo shiriki michuano ya Ulaya ambapo zenyewe ndiyo zitashiriki uko kwenye UEFA Europa Conference League (UECL).

Uingereza itashiriki timu moja itakayomaliza nafasi ya 7.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents