Burudani

Ali Kiba adai alianza kuonyesha anapenda muziki akiwa na siku 7

Staa wa muziki Ali Kiba amesema wazazi wake walikiona kipaji chake cha muziki toka akiwa mchanga.
Ali Kiba

Akiongea na Chill na Sky hivi karibuni, Kiba amesema aliambiwa alianza kucheza muziki akiwa na siku saba.

“Unajua mimi zamani kidogo wakati nazaliwa, nimeanza kucheza muziki nikiwa na siku saba. Nimeambiwa nilikuwa nikisikia muziki nacheza, mimi kitanda changu baba yangu alininunulia kutoka Nairobi, kilikuwa kina radio, lazima waweke station ambayo inapiga muziki hapo ndio naweza kulala, ikizimwa nalia,” alisema Ali Kiba.

Aliongeza, “Kwa hiyo nilikuwa mpenzi wa muziki kutoka kipindi hicho na mpira ukaja baadae, nikawa nacheza nyumbani, shuleni baadae nikawa vizuri kabisa,”.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents