Michezo

Alichokisema Zinedine Zidane baada ya kufungwa na Spurs

Hapo jana usiku michuano ya Klabu bingwa Barani Ulaya iliendelea katika viwanja mbali mbali huku mabingwa watetezi Klabu ya Real Madrid ikiwa ugenini nchini Uingereza imekubali kipigo cha mabao 3-1 dhidi ya wenyeji wao timu ya Tottenham Hotspur.

Mara baada ya kumalizika kwa mchezo huo meneja wa Madrid, Zinedine Yazid Zidane “Zizou” katika mazungumzo yake na waandishi wa habari amesema kuwa hashangazwi na matokeo aliyopata dhidi ya Spurs kwakuwa timu hiyo ilikuwa imekamilika na bora zaidi kuliko wao.

“Haya ni maisha tu ni ukweli lazima Real ibadilike na kurudi katika kiwango chake ilichokuwanacho hapo hawali,”amesema Zidane anaetambulika kwa jina la utani la Zizou.

Zidane  ameongeza “Hapana sihofii na kamwe sitohofia kwa chochote kitakachotokea msimu huu. Usiku waleo tutafanya uchambuzi lakini tumekutana na timu bora ambayo imekuja kucheza vizuri zaidi yetu lazima tuheshimu hilo.”

“Katika upande wa nafasi bado nitasema tumecheza na timu bora  kiujumla na wala sihofii kuona tumekosa magoli tunachohitaji ni kuonyesha kuwa tunauzoefu na ni mabingwa hivyo tutalazimika kubadili muelekeo tunaokwenda nao.”

“Ninachoweza kusema tunapaswa kujilinda na hatuwezi kuwa na furaha na matokeo yaliyopatikana kwa wakati huu mashabiki wetu hawawezi kujiskia vizuri hivyo ni kipindi kibaya kwetu.”

Magoli ya hapo jana usiku katika Uwanja wa Wembley yamefungwa na Dele Alli akiyetupia mawili na Christian Eriksen akipiga moja kwa upande wa Spurs wakati Ronaldo akifunga moja na kupelekea matokeo kuwa 3-1 hivyo Tottenham Hotspur imetinga hatua ya 16 bora.

Wakati Madrid italazimika kushinda michezo miwili iliyobaki ili kupata nafasi ya kuendelea katika michuano hiyo ya klabu bingwa Brani Ulaya.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents