Burudani

Alikiba atajwa kuwania tuzo za MTV EMA 2016

Alikiba ametajwa kuwania kwenye tuzo za mwaka huu za MTV Europe Music Awards (EMA) kipengele cha Best African Act.

kiba

Anakuwa msanii pekee kutoka Afrika Mashariki kutajwa kuwania kipengele hicho. Kiba atachuana na wasanii wengine wakiwemo Wizkid na Olamide wa Nigeria na Black Coffee na Cassper Nyovest wa Afrika Kusini.

Kama ilivyokuwa mwaka jana, mshindi katika hatua ya kwanza ataendelea kwenda kuwania kipengele cha Worldwide Act: Africa/India ambacho mwaka jana alishinda Diamond Platnumz.

Bonyeza hapa kwenda kumpigia kura Alikiba.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents