Siasa

Aliyewahi kuwa mlinzi wa Mbowe atangaza nia CCM, aeleza sababu za kufanya hivyo (+Video)

Zoezi la Urejeshaji fomu kwa watia nia wa kugombea nafasi za Ubunge na Udiwani kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), limekamilika leo ambapo takwimu zinaonesha vijana wengi wamejitokeza zaidi kuliko miaka iliyopita.

Aliyewahi kuwa mlinzi wa Freeman Mbowe, Erick Mandia akirejesha fomu.

Kwa mujibu wa EATV imeshuhudia aliyewahi kuwa Red Brigedi Kamanda CHADEMA Taifa na mlinzi wa karibu wa Mwenyekiti wa chama hicho Freeman Mbowe, Erick Mandia, akirejesha fomu katika ofisi za CCM Kata ya Mbezi Juu, Kinondoni jijini Dar es salaam ambapo anaeleza sababu za kutogombea CHADEMA na kuhamia CCM kuwa ni kuridhishwa na sera za Rais Magufuli.

“Nimekuja CCM kukitumikia chama na hata ikitokea sikupata nafasi ya kuteuliwa kuwa mgombea wa Udiwani hapa, niko tayari kusimamia amani na kumuunga mkono mgombea atakayepitishwa”, amesema Erick Mandia.

Zoezi hilo limefanyika kwa siku nne kuanzia Julai 14, 2020, kama alivyotangaza Katibu mwenezi wa CCM Humphrey Polepole.

https://www.instagram.com/p/CCxpqmIhKYQ/

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents