Burudani

Harmonize atangaza balaa, Kutambulisha wasanii watatu kwa wakati mmoja

Msanii wa muziki wa bongo Fleva na CEO wa Konde Gang Harmonize ametanagza kuwa atatambulisha wasanii watatu mwezi wa nane (August)

Kupitioa ukurasa wake wa Instagram msanii huyo ametangaza ujio huo wa wasanii watatu kupia lebo yake ya Konde Gang, Hadi hivi sasa lebo hiyo tayari imemtambulisha msanii mmoja ambaye ni Ibrah na tayari ameachia nyimbo nyingi ikiwemo EP yake ya kwanza ya STEP ambayo ilikuwa na nyimbo tano tu.

Nyimbo zilizopo kwenye hiyo EP ni:-

1. ONE NIGHT STAND. Ibraah ft Harmonize

2.WANDOTO

3. WAWA. Ibrah Ft Joeboy

4. SUBIRA. Ibrah ft Skiibii

5. NANI

Mbali na hiyo EP Ibrah alitoa ngoma yake ya kwanza ambayo ilifanya vizuri sana akiwa chini ya Konde Gang ya NIMEKUBALI.

Hivyo endapo wasanii hao watatambulishwa Konde Gang itakuwa na jumla ya wasanii watano, Wa kwanza akiwa Harmonize, wapili Ibrah na hao wengine watatu wanaotarajiwa kutambulishwa.

https://www.instagram.com/p/CCwXUZvHlJT/?igshid=jl9461nqqv33

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents