Michezo

Anthony Joshua Vs Wladimir Klitschko waipa shavu Sky Sports kushinda Broadcast Awards

Kituo cha michezo cha Sky Sports chatajwa kuwa ‘Best Sports Programme’ kutoka Broadcast Awards kufuatia kufanikiwa kuwafikia watu wengi zaidi wakati wa maandalizi ya pambano lao waliloliandaa baina ya   Anthony Joshua dhidi ya Wladimir Klitschko.

Pigano hilo lililoshuhudiwa Joshua akitwaa taji la uzito wa juu kwa TKO raundi ya 11 linakadiriwa kufuatiliwa na mamilioni ya watu.

Wadau mbali mbali wakiwa wameudhuria tukio hilo la Broadcast Awards

Katika vipindi bora sita vya michezo vilivyoingia katika kinyang’anyiro hicho Sky Sports imefanikiwa kuingiza vinne ambavyo ni Anthony Joshua Vs Wladimir Klitschko, Monday Night Football, Abu Dhabi Grand Prix na Lions Tour.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents