Habari

Apeleka Maiti ya Mjomba wake Benki ili apatie Mkopo Benki

Polisi nchini Brazil wanamshikilia Erika De Souza Vieira kwa tuhuma za kupeleka maiti ya mjomba wake Paulo Roberto Braga (68) Benki ili achukue mkopo kwa jina lake ambao ni Dola 3,250 za Kimarekani sawa na Shillings Milioni Nane za Kitanzania.

Muda mfupi baada ya Erika kuingia katika moja ya Benki huko Rio de Janeiro akiwa na mwili huo wa mjomba wake alikamatwa na ameshtakiwa kwa kosa la kukiuka sheria inayolinda maiti na kujaribu kuiba na kujipatia pesa kwa njia ya Ulaghai.

Picha ya Video ilipandishwa na kituo cha televisheni na Aljazeera inamuonesha mwanamke huyo akimshikisha kalamu marehemu huyo na kumsihi aweke saini kwenye karatasi ya benki huku pia akiwa ameshikilia kichwa chake.

Maofisa wa benki walishtuka baada ya kuona mwili wa mteja huyo ukiwa umepauka sana na nido waliposema hayupo sawa.

Polisi nchini Brazil wanaendelea na uchunguzi wa tukio hilo ili kufahamu pia kuna watu wengine wanaohusika.

 

 

 

 

 

 

cc:Tanzaniaweb.Live

Imeandikwa na Mbanga B.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents