Habari

Apple yakiri kuwa betri za iPhone 5S zinaishiwa chaji haraka, yasema itawapatia simu mpya wateja walioathirika

Je unamiliki simu mpya ya iPhone 5S na unahisi inatatizo la betri kuishiwa chaji kwa muda mfupi? Kampuni ya Apple watengenezaji wa smartphone za iPhone imekiri kuwepo kwa tatizo la betri kuwahi kuisha chaji katika simu za iPhone 5S ambazo zimeingia sokoni rasmi hivi karibuni.

iphone-5s

Msemaji wa Apple Teresa Brewer amesema kuwa tatizo hilo ni matokeo ya kasoro za kiwandani zinazosababisha simu kuishiwa chaji kwa muda mfupi zaidi ya inavyotakiwa. Amedai kuwa tatizo hilo limeathiri idadi ndogo tu ya simu hizo na kusema kuwa wamiliki wa simu hizo chache watabadilishiwa.

Brewer aliongeza kuwa Apple inawasiliana na wateja wake wachache ambao wana iPhone 5S zenye tatizo hilo ili waweze kuwapatia simu mpya.

Hapo awali simu za iPhone 5S zilidaiwa kuwa na uwezo wa kutumika kwa masaa 10 kwa kuongea na masaa 250 ikiwa standby na chaji mstari moja.

Idadi ya Simu milioni tisa za iPhone 5S zimeshauzwa mpaka sasa toka zilipozinduliwa mwezi September.

Source: Mail Online

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents