Habari

Arusha: Mfanyabiashara mbaroni kwa tuhuma za kumpiga chupa mkewe mbele ya baba mkwe

Mfanyabiashara maarufu wa madini jijini Arusha, Venance Moshi (30)amefikishwa Mahakamani na kusomewa maelezo ya awali katika kesi inayomkabili ya kushambulia na kumjeruhi mkewe kwa chupa usoni wakiwa wanasuluhishwa mgogoro wa ndoa yao na baba wa mwanamke.

Mbele ya hakimu, Devota Msofe wa mahakama ya wilaya Arusha ,mwendesha mashtaka wa serikali, Agnesi Hyera alieleza mahakama hiyo kuwa mnamo Machi 11 mwaka 2016 katika maeneo ya Moshono kwenye usuluhishi wa mgogoro wa ndoa yao ,mshtakiwa alinyanyua glasi na kumpiga kwenye jicho la kulia mlalamikaji (mkewe) Agnesi Joseph (30)iliyomjeruhi vibaya .

Mwendesha mashitaka aliieleza mahakama hiyo kuwa kuwa hatua hiyo ilimsabishia mlalamikaji atokwe na damu nyingi na baadaye kutoa taarifa kituo cha polisi ambapo mtuhumiwa alitiwa mbaroni na baadaye kufikishwa mahakamani.

Baada ya mashtaka hayo kusomewa mshitakiwa alikana mashtaka, Hakimu Msofe alipanga siku ya kuanza kusikilizwa kwa shauri hilo,baada ya upande wa Jamhuri kudai kuwa wapo tayari kwa usikilizwaji wa kesi hiyo. Upande wa jamhuri unatarajia kuwasilisha mashahidi watatu na vielelezo kadhaa ikiwemo hati ya polisi(PF3) , hati ya daktari pamoja na picha za jeraha.

Kesi hiyo imepangwa kusikilizwa Februari 6, mwaka huu, saa tatu asubuhi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents