Habari

Askari polisi walioiba bunduki watupwa jela

Aliyekuwa Mkuu wa Kikosi cha Polisi cha Kutuliza Ghasia (FFU), Mkoa wa Tabora, Bhoke Bruno na wenzake saba jana Jumatano tarehe 6 Novemba 2017 walihukumiwa kifungo cha miaka 15 jela kwa kosa la kuiba bunduki nane aina ya SMG, mali ya mwajiri wao.

Wengine waliohukumiwa kifungo katika hukumu iliyosomwa na Kaimu Msajili wa Mahakama Kuu Kanda ya Tabora na Sharmira Sarwatt ni Koplo Idd Abdalah, PC Mwinyi Gonga na Said Mgonela, wote kutoka kikosi cha FFU Tabora.

Waajiriwa hao wa jeshi la polisi kwa pamoja walitiwa hatiani kwa makosa matatu ya kula njama, kuiba na kushindwa kuzuia tukio.

Mahakama pia iliwapa adhabu kama hiyo washtakiwa wengine watatu Shaban Haruna, Shaban Kabanika na Idd Supu waliodaiwa kushirikiana na waliokuwa maofisa hao wa polisi.

Washitakiwa wengine watatu kati ya 10 waliokuwa wakishtakiwa, Charles Abihud, Emmanuel Festo na Nicholaus Mlelwa, waliachiwa huru baada ya ushahidi dhidi yao kukosekana.

Ushaihidi uliowasilishwa na upande wa Jamhuri umeithibitishia Mahakama pasipo shaka kuwa washtakiwa saba kati ya 10 walihusika na makosa yanayowakabili, hivyo wanahukumiwa kifungo cha miaka mitano kwa kila kosa,” amesema Sarwatt.

Awali upande wa mashtaka ulioongozwa na Wakili Mwandamizi wa Serikali, Juma Masanja uliiambia Mahakama kuwa kwa pamoja, wahtakiwa walitenda makosa hayo kati ya Aprili 2013 hadi Aprili 2014.

Chanzo:Mwananchi

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents