Burudani

Baada ya kuzingua kwa muda mrefu, Keri Hilson atangaza kuja Afrika Mashariki kutumbuiza

Kwa wadau wa burudani hususani ya muziki, toka mwaka 2012 kulikuwa na habari kuwa Msanii wa muziki kutoka Marekani, Keri Hilson atakuja Tanzania kutumbuiza kipindi hicho anatamba na ngoma yake ya  Knock You Down lakini show hiyo iliishia kwenye mitandao tu kwani mrembo huyo hakuja Tanzania.

Keri Hilson

Sasa kama bado unahamu ya kumuona msanii huyo jukwaa akitumbuiza basi habari njema ni kwamba Mrembo huyo ametangaza rasmi kupitia ukurasa wake wa Twitter kuwa atakuwa na show nchini Kenya mwezi Agosti 3, 2018.

Hii itakuwa ni mara yake ya kwanza kutumbuiza nchini Kenya tangu mwaka 2011 alipotangazwa kutumbuiza kwenye fainali ya mashindano ya Tusker All Stars Project Fame.

SOMA ZAIDI – Homeboyz wamshataki promoter ‘fake’ wa Keri Hilson

Keri Hilson pia mwaka 2012 kupitia ukurasa wake wa Twitter alitaganza kuwa atakuja kutumbuiza Tanzania lakini show hiyo mpaka leo haijajulikana ilipotelea wapi.

SOMA ZAIDI – Show ya Keri Hilson Tanzania imeishia wapi?

Kwa hiyo ujio wa Keri Hilson nchini Kenya utakuwa ni wa kihistoria na pengine huenda ikawa ni kulipa fadhila kwa mashabiki wake.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents