Habari

Show ya Keri Hilson Tanzania imeishia wapi?

Keri+Hilson

Wiki kadhaa zilizopita mwanamuziki wa kike wa nchini Marekani alithibitisha kupitia Twitter kuwa katikati ya mwezi huu wa December angekuwa na show nchini Tanzania na Kenya.

Keri-Hilll

Mpaka leo hakuna dalili zozote za msanii huyo kuja. Haikuweza kubainika mara moja nani waliokuwa wamezungumza naye kwaajili ya show hizo na nini kimetokea mpaka zisifanyike mpaka sasa. Wiki kadhaa pia Keri alikuwa na show nyingine nchini Nigeria ambayo hata hivyo mahudhurio yake hayakuwa ya kuridhisha kiasi cha kuonesha wazi kuwa waandaaji wa show hiyo walikula hasara.

Kama Keri hatokuja Tanzania na Kenya huenda hiyo itakuwa ni sababu moja ya kubwa ya waandaaji kutoendelea na mipango ya kumleta mrembo huyo Afrika Mashariki.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents