Michezo

Balaa lingine tena, Simba SC uso kwa uso na Yanga SC michuano ya Kagame Cup

Klabu mbili mahasimu kutoka Tanzania, Simba na Yanga zimepangwa kundi moja kwenye michuano ya Kombe la Kagame inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi Juni 28 hadi Julai 13, 2018 .

Rais wa TFF katikati kwenye picha, Wallace Karia.

Timu hizo zimepangwa kundi C ambapo zimeungana na klabu nyingine za St. George kutoka Ethiopia na Dakadaha Somalia.

Makundi hayo ya michuano ya Kagame Cup yametangazwa leo na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na makundi mengine ni kama ifuatavyo hapa chini.


Bingwa wa michuano hiyo atapata Dola $30,000 sawa tsh. milioni 68.4 na Mshindi wa pili Dola $20,000 ambazo ni sawa na milioni 45 huku mshindi wa tatu akiambulia Dola $10,000 sawa na milioni 22 za kitanzania.

Michuano ya CECAFA Kagame Cup kwa mwaka huu yanafanyika nchini Tanzania na yatarushwa mubashara na Azam TV.
https://youtu.be/zkxYOjwS_ws

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents