Michezo

Balotelli asikitishwa na vitendo vya kibaguzi baada ya kubaguliwa nchini Ufaransa

Mchezajiwa wa klabu ya Nice ya nchini Ufaransa Mario Balotelli anasema kuwa alikuwa mwathiriwa wa ubaguzi wa rangi wakati wa mechi ya Ijumaa dhidi ya Bastia.

Balotelli ambaye mchezaji hyo wa zamani wa Liverpool mwenye umri wa mika 26 aliandika katika mtandao wa kijamii akisema, ni jambo la kawaida kwamba wafuasi wa Bastia hufanya makelele ya tumbili kwa mechi yote na hakuna mtu katika idara ya adhabu anayechukua hatua?

”Kwa hivyo ubaguzi wa rangi ni sheria halali nchini Ufaransa? Ama ni Bastia pekee? Soka ni mchezo mzuri lakini watu kama wafuasi wa Bastia wanaharibu.Ni aibu kubwa”.

Balotelli ambaye alicheza dakika 90 aliporudi uwanjani baada ya kutumikia adhabu yake ya mechi waliyo toka sare ya 1-1 huko Corsica.

Ujumbe huo uliotumwa katika mtandao wa Instagram ulisambazwa na Nice katika mtandao wa Twitter wa klabu hiyo.

Jopo la adhabu la ligi ya Ufaransa ambalo hutoa maamuzi halijatoa tamko lolote.

Balotelli amesha funga mabao 10 katika mechi 15 tangu alivyo jiunga na Nice.

Source: BBC

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents