Habari

Balozi wa China, Israel afariki dunia

Balozi wa China nchini Israel, Du Wei, amefariki dunia akiwa nyumbani kwake katika mji wa Tel -Aviv kulingana na maafisa wa polisi wa Israel na vyombo vya habari.

Chinese ambassador to Israel found dead at Herzliya home - www ...

Bwana Du, mwenye umri wa miaka 57 amekutwa ameaga dunia katika kitanda chake na sababu ya kifo chake bado haijajulikana.

Alikuwa ameteuliwa kuwa balozi mwezi Februari 2020 baada ya kuhudumu kama balozi wa China nchini Ukraine.

Balozi huyo alikuwa ameoa na alikuwa na mtoto wa kiume lakini familia yake haijulikani iwapo ilikuwa nchini humo.

Alikuwa akiishi katika mtaa wa Herzliya mjini Tel Aviv. Msemaji wa polisi nchini Israel aliambia chombo cha habari cha Reuters : Kama taratibu za kawaida maafisa wa polisi tayari wamefika katika eneo la tukio.

Runinga ya Israel Channel 12, ilinukuu vyanzo vya matibabu vilivyosema kwamba balozi huyo alifariki akiwa usingizini.

Katika ujumbe uliochapishwa katika tovuti ya ubalozi huo , muda tu baada ya uteuzi wake wa kuwa balozi, bwana Du aliusifu uhusiano kati ya China na Israel.

Siku ya Ijumaa, ubalozi wake ulimshambulia waziri wa maswala ya kigeni nchini Marekani Mike Pompeo ambaye alikuwa ameikosoa China kwa jinsi ilivyokuwa inalishughulikia suala la virusi vya corona wakati wa ziara yake nchini Israel.

Katika chapisho lake lililowekwa katika gazeti la Jerusalem Post, ubalozi huo uliyashutumu matamshi ya bwana Pompeo kama ‘upuuzi’ , na kukana madai kwamba China ilificha kuhusu mlipuko huo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents