Michezo

Barca yainyoosha PSV, Messi apiga hat-trick na kuwa man of the match

Mshambuliaji hatari ndani ya klabu ya Barcelona, Lionel Messi ametupia magoli matatu ‘hat-trick’ na kuiwezesha timu yake kuchomoza na ushindi wa jumla ya mabao 4-0 dhidi PSV mchezo wa ufunguzi michuano ya klabu bingwa barani Ulaya.

Messi ambaye ni nahodha wa Barca akiwa kwenye uwanja wa nyumbani Camp Nou ameifungia timu yake bao la kwanza safi kabisa dakika ya 31 kipindi cha kwanza kupitia mpira wa ‘free-kick’.

Hata hivyo nyota huyo raia wa Argentina akaifungia Barcelona bao la pili dakika ya 77 na la tatu dakika ya 87 huku, Ousmane Dembele akipachika bao lake dakika ya 74.

Katika mchezo huo uliyokuwa na burudani ya kutosha umeshuhudiwa mchezaji wa Barca, Samuel Umtiti akitolewa nje kwa kadi nyekundu baada yakupewa kadi ya pili ya njano kwa kumchezea vibaya, Hirving Lozano.

Na hivyo mchezo huo wa kundi B kumalizika kwa kuishuhudia miamba hiyo ya soka Hispania ikichomoza na ushindi huo mnono wa mabao 4-0.

Wachezaji wa Barcelona, Ter Stegen (6), Pique (7), Alba (7), Roberto (7), Umtiti (5), Rakitic (7), Busquets (7), Coutinho (7), Suarez (8), Messi (9), Dembele (8).

Wachezaji wa akiba, Lenglet (n/a), Arthur (n/a), Vidal (n/a).

Wachezaji wa kikosi cha PSV Eindhoven, Zoet (7), Dumfries (7), Schwaab (6), Viergever (6), Angelino (6), Roasrio (6), Hendrix (7), Pereiro (6), Bergwijn (7), De Jong (7), Lozano (7).

Wachezaji wa akiba,Isimat-Mirin (4), Malen (4), Gutierrez (n/a).

Wakati nahodha wa Barcelona, Lionel Messi akiibuka kuwa mchezaji bora wa mechi hiyo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents