Bongo Movie

Batulli, Ndauka, Richie na Slim wachaguliwa kuwa mabalozi wa soko la hisa la Dar es Salaam, DSE

Waigizaji wa filamu nchini Yobnesh Yussuph maarufu kama Batulli, Rose Ndauka, Single Mtambalike na Slim Omary wameteuliwa kuwa mabalozi wa soko la hisa la Dar es Salaam, DSE.

Batulli
Kutoka Kushoto: Rose Ndauka, Slim Omary, Single Mtambalike na Batulli

Batulli ameiambia Bongo5 kuwa mkataba wa ubalozi wao utadumu kwa kipindi cha miezi tisa.

“Kazi yetu ni kutangaza vipindi vya soko la hisa la Dar es salaam tukiongozwa na Pascal Mayala, matangazo yote tutakuwepo TV, radio na magazeti,” amesema Batulli.

Batu
Batulli

“Nimejisikia vizuri sana ni kazi ya heshima kubwa sana kwangu na naamini itanifanya niwe na kipaji kipya cha utangazaji,” aliongeza Batulli.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents