Burudani

Belle 9 atoa sababu za kutopenda kumuonesha sana mwanaye mtandaoni kama mastaa wengine

Muimbaji Belle 9 ni baba wa mtoto mmoja wa kiume, lakini ana mtazamo tofauti kuhusu style ya mastaa kuwaonesha sana watoto wao wadogo kwenye mitandao ya kijamii.

BELLE 9

Muimbaji huyo mwenye makazi yake Morogoro, amesema kuwa yeye binfasi ameshawahi kumuonesha mtoto wake ambaye kwa sasa ana miaka miwili, lakini hapendi kumuonesha sana kwasababu anamuheshimu na hajui atapenda kuwa nani baadae.

“Mimi sijafanya sana hivyo kwasababu sijajua mwanangu atakuja kuwa mtu wa aina gani, nimependa tu kumpa nafasi yake na namuheshimu kama yeye na naheshimu uwepo wake, sijui atakuja kuwa nani… “ aliiambia Bongo5.

Aliendelea,
“Mimi wazazi wangu kwamfano mama yangu mimi ni mtu wa dini, kwahiyo kama angetaka kuniweka katika image kama hiyo labda kunifanyia kama mimi navyomfanyia mtoto labda kumuonesha mtoto wangu, sijui yeye atakuja kuchagua kitu gani badae, sasa mama yeye anaimba kwaya mimi naimba Bongo fleva si unaona…sijui mtoto wangu atakuja kuwa nani sasa maswala ya kuanza kumuonesha onesha anaweza akaja labda asipende baadae ndio maana sipendi kumuonesha sana mtoto.” Alimaliza Belle 9.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents