Habari

Binti aliyetekwa na Boko Haram asimulia kisa cha kutumwa kufanya mashambulizi ya kigaidi

Mmoja ya msichana aliyetekwa na kundi la Boko Haram, ameelezea kisa cha jinsi alivyoteuliwa kufanya shambulio la kigaidi baada ya kukataa kuolewa na waasi wa Boko Haram.

Msichana huyo mwenye miaka 14 , aliteuliwa kufanya ugaidi na kundi la Boko Haram kufuatia kukataa kuolewa na mmoja wa makamanda wa kundi hilo. Binti huyo alitekwa akiwa na baba yake mzazi katika jimbo la Borno mwaka 2013. ‘Nimesalia kwa zaidi ya miaka mitatu katika mikono ya Boko Haram. Wafuasi watatu tofauti wa kundi hilo walijitokeza wakitaka kunioa lakini nikakataa” alieleza msichana huyo.

Binti huyo alizidi kufafanua kuwa, wawili kati yao waliotaka kumuoa walikuwa makamanda katika jeshi hilo la ugaidi. Anasimulia kwamba aipokataa kwa mara ya tatu , ndipo kamanda mmoja alipokasirika na kumitishia kumuua yeye na baba yake.

Kufuatia kukataa kuolewa, msichana huyo ameeleza kuwa baada ya wiki moja, ndipo aliamuriwa kwenda Maiduguri, kaskazini mwa Nigeria, kwa ajili ya kufanya mashambulizi,huku akiwa amechomwa shindano ya usingizi. Hata hivyo binti huyo hakuweza kutekeleza shambulio hilo kwani aliweza kujisalimsha na kutoa mkanda wa mabomu.

Na Laila Sued

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents