Habari

Black Rhino yuko juu!!

Black Rhino yuko juu!!
Tunapenda kukuhabarisha kwamba, msanii Black Rhino bado anaendelea
kukamata chati za juu kunako Kituo cha Televisheni cha Channel O cha
Afrika Kusini kupitia video ya ngoma yake, Black Chata

Rhino alithibitisha hilo kwa kusema kwamba, wiki ya pili sasa video hiyo inakamata namba moja kunako Top 10 na Top 100 za tv hiyo huku ikizipoteza video vya mastaa mbalimbali wanaofanya muziki Marekani kama Wycleaf Jean na wimbo wake ‘Touch your Button’, huku Alicia Keys na video ya wimbo wake, ‘Another Way to die’ akiambulia nafasi ya 11 na wengine kibao.

“Hiyo inaonesha ni jinsi gani muziki wetu unavyozidi kwenda mbali zaidi. Julai mwaka huu namalizia digree yangu ya Biashara na Masoko hapa Chuo Kikuu cha Mzumbe, Morogoro kisha naingia kwenye mchakato wa muziki rasmi”, alisema Rhino.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents