Makala

#Bongo5hamasa: Toka geto usione aibu pigania ndoto zako, hakuna anayejali maumivu yako

Toka ghetto,nenda nje ya akili yako kamilisha mipango yako. kuamka kutoka kuchangamana na watu kuna fungua akili kuangalia fursa zilizo mbele yetu.

Tunaishi ndani ya akili zetu wakati uliopita na ujao. Wakati huu tulionao sasa tumefichama tukijisemea watanidharau watanionaje ni kianzia chini au nikianza upya.

Muda mwingi tunatumia kuwaza kubuni kuchagua na kupangilia mambo mbali mbali juu ya maisha yetu . Haya yote huanza tukiwa tumetulia ndani huku tukipitia maumivu ya kukosa.

Haya yote huishia akilini ,tukitoka ghetto tunavuta hewa safi ,stori na wana kisha tunarudi kuendelea na maumivu yetu kama kawaida.

Hatuwezi kutoka kwenda nje ya gheto na akili yako kutafuta kukamilisha tuliyoyaanza akilini.

Hakuna anayejali ndoto zako , maumivu na njaa yako .jionee haya wewe mwenyewe,toka getto kamilisha. Usione aibu kuanzia hapo ulipo na ulichonacho .

Ndio watakudharau,dharau huwa za kitambo tu tunao msemo “wanaokudharau siku moja watakusalimia kwa heshima”. Usiogope pambana.

#Bongo5hamasa imeandaliwa na @tujuavyo and @el_mando_tz

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents