Michezo

Chelsea yavuliwa ubingwa wa Capital One na Stoke City

Matokeo mabaya yanaendelea kumuandama kocha Jose Mourinho msimu huu baada ya vijana wake wa Chelsea kuvuliwa ubingwa wa kombe la Capital One na Stoke City kupitia mikwaju ya penati kwenye mechi iliyochezwa Jumanne hii.

151028060111_chelsea_hazard_league_cup_512x288_ap

Stoke City walipata goli lao la kwanza kupitia mchezaji wao Jonathan Walters dakika chache baada kipindi cha pili. Lakini Loic Remy aliyeingia kuchukua nafasi ya Diego Costa aliyetoka baada ya kuumia, aliisawazishia goli Chelsea katika dakika ya 90.

Stoke wamesonga mbele kwenye raundi ya tano ya michuano hiyo kwa ushindi wa penati 5-4 kufuatia sare ya kufungana goli 1-1.

chelsea-hoi-3-e1446010766484

Winga wa kimataifa wa Ubelgiji Eden Hazard alikosa penati iliyoifanya Chelsea kutupwa nje ya mashindano hayo.

Kuvuliwa huko kwa ubingwa kwa Chelsea ni habari mbaya kwa kocha Jose Mourinho ambaye hana kwa sasa. Sasa anasubiri hatima yake dhidi ya Liverpool Jumamosi ijayo kuona kama ataendelea kuwa meneja wa Chelsea.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents