Bongo Movie
Chocolate Flavour ndani ya Movie
Raisi wa Masharobaro aka Mr. Chocolate Flavour, anatarajia kuachia ‘track’ mpya itakayokwenda kwa jina la ‘Ng’ombe’.
Amesema wimbo huo utakuwa kwenye albamu yake ya kwanza itakayoshikilia nyimbo sita. Akizitaja nyimbo zitakazokuwa kwenye Albamu yake ya kama Oyo oyo, Ng’ombe, Singa singa, Pamela, Safari, Sina dola na Bingwa wa makopa.
Pia alidokeza kwa kusema mwaka huu ana matarajio mapya kabisa ya kuibua vichwa vipya, katika muziki wa bongo Fleva ukiachana na Diamond wa ‘Mbagala’, Top C wa ‘Rofa’, na wengine wengi.
Rais huyo amedokeza kuwa na mikakati mapya ya kujiingiza kwenye ‘Movies’ kwa kudondosha filamu yake itakayoenda kwa jina la ‘Welcome Sharobaro’, ila kwa sasa amejitupa kushiriki katika filamu ya Jackline Wolper.