Burudani

Christian Bella kufanya show 4 mfululizo Australia

Mkali wa masauti Christian Bella weekend hii anatarajia kufanya show 4 mfululizo katika miji tofauti nchini Australia.

Akiongea na Bongo5 wiki hii, Bella amesema show hizo zitamfungulia milango mipya ya soko la muziki wake nchini Australia.

“Kwa sasa nipo Australia kwajili ya maandalizi ya tour yangu kwa sababu nitakuwa na show nne mfululizo kwa hiyo maandalizi yalikuwa yanahitajika,” alisema Bella. “Unajua tunafanya show nje siyo tu kwajili ya kupata pesa peke yake, sisi ni wasanii lazima tutafute masoko mpya kwahiyo hii naichukulia ni kama promotion,”

Muimbaji huyo ambaye anafanya vizuri na wimbo ‘Ollah’ atakuwa na show Sydney tarehe 21 April, Perth tarehe 22 April, Melbourne tarehe 28 April na Brisbane 29th April.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents