Habari

‘Mh Rais, majipu unayotumbua wewe ni madogo madogo’ – Askofu

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli na Mkewe Mama Janeth Magufuli sikukuu ya Pasaka, waliungana na waumini wa kanisa la Africa Inland – Tanzania Dayosisi ya Pwani Pastorate ya Magomeni kusali ibada ya Pasaka.

Katika ibada hiyo Askofu wa Kanisa la Africa Inland – Tanzania Baba Askofu Charles Salalah aliongoza maombi ya kumuombea Rais Magufuli na kumpongeza kwa kazi kubwa ya kurekebisha mambo yote yasiyofaa nchini ikiwemo kuwaondoa viongozi wanaotumia madaraka yao vibaya na kufuja mali za umma.

“Jipu mama ni dhambi. Mheshimiwa Rais unafanya kazi kubwa ya kutumbua majipu. Majipu unayoyatumbua wewe ni majipu madogo madogo yaliyotokana na jipu kuu ambalo ni dhambi za mwanadamu, na jipu hili lilitumbuliwa na Bwana Yesu miaka kama 2000 iliyopita. Kwa hiyo sisi wakristo wenzako na waumini wengine tunakuombea sana na tunakuunga mkono katika kazi ya kutumbua majipu haya madogomadogo ya watumishi hewa, mishahara hewa, mikopo hewa na mengine mengi ambayo ni hewa ” alisema Askofu Salalah.

Aidha Rais Magufuli katika ibada hiyo aliwashukuru Wakristo wa Kanisa la Africa Inland na waumini wa madhehebu mengine ya dini kwa kuendelea kumuombea.

Na Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents