Burudani

Common aachia video ya wimbo wa kupinga mauaji ya watu weusi Marekani

Rapper kutoka mji wa Chicago nchini Marekani, Common ameachia video ya wimbo wake wa ‘Black America Again’ aliomshirikisha Stevie Wonder ambao unaopinga mauaji ya watu weusi yanayoendelea nchini humo.

common-epix

“Here we go again,” amerap Common kwenye wimbo huo. “Trayvon will never grow to be an older man / Black children, they childhood stole from them / Robbed of our names and our language, stole again.”

Wimbo huo utapatikana kwenye albamu ya 11 ya msanii huyo anayotarajia kuiachia hivi karibuni.

Mpaka sasa ni zaidi ya watu watano weusi wameuawa na polisi wa kizungu nchini humo kuanzia mwezi Julai, mwaka huu akiwemo Philando Castile, Alton Sterling na tukio jingine lililotokea siku chache zilizopita kwenye mji wa Charlotte kwa Keith Lamont Scott kupigwa na risasi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents