Habari

Viongozi wa dini wadai gazeti la Tanzania Daima limetoa taarifa ya uongo

Viongozi wa dini wamepinga taarifa zilizochapishwa na gazeti la Tanzania Daima Septemba 21 zinazodai kuwa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Magufuli amekataa kuonana na viongozi hao.

fullsizerender_1-702x336

Gazeti hilo lilichapisha taarifa hiyo iliyokuwa na kichwa cha habari kinachosomeka, “Magufuli awatosa viongozi wa dini”. Akiongea na waandishi wa habari Ijumaa hii ofisini kwake, Sheikh wa mkoa wa Dar es Salaam Alhad Mussa Salum amesema taarifa hizo si za kweli.

“Taarifa hizo si za kweli, zimelenga kumgombanisha rais na viongozi wa dini na watanzania kwa ujumla na hilo halitafanikiwa,” alisema Sheikh Alhad. “Naomba watanzania wasisikilize maneno hayo kwasababu hayana nia njema kwa taifa letu. Naamini Mh. rais tutaonana naye na tutaongelea mustakbali wa nchi katika mambo mbalimbali.”

Sheikh Mussa ameongeza kuwa uamuzi wao huo wa kuonana na Rais Magufuli haujatokana na kuagizwa na viongozi wa UKAWA bali ni maono waliyopewa na Mungu.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents