Michezo

David Beckham akiri kushtushwa na usajili wa Sanchez asema haya

Mchezaji wa zamani wa klabu ya Manchester United na timu ya taifa ya England, David Beckham amezungumzia usajili wa Alexis Sanchez kutua katika timu hiyo akitokea Arsenal.

Nahodha huyo wa zamani wa England amemzungumzia mchezaji huyo wakati wa uzinduzi wa klabu yake Miami huko nchini Marekani, “Mpaka sasa nashindwa kuamini kwa kile kilichotokea hakika,” amesema Beckham.

Beckham ameongeza “Wakati alipokuwa sehemu ya timu kubwa kama ya Arsenal na mara ghafla akaama kwa muda mchache tu na kuelekea kaskazini katika klabu kubwa ni ajabu kushuhudia hilo.”

“Sote tunamtakia mafanikio, mimi ni shabiki wa Manchester United hivyo ninafurahi kuona timu yangu imefanikiwa kumpata mchezaji mwenye uwezo na kipaji kama yeye,”

 Mshambuliaji huyo raia Chile mwenye umri wa miaka 29 ametua United mwanzoni mwa juma lililopita huku akifanikiwa kulipwa paundi 600,000 kwa wiki mshahara paundi 350,000, haki ya matangazo paundi 100,000 na paundi 144,000 kama nyongeza.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents