BurudaniDiamond Platnumz

Diamond aingia studio na Fally Ipupa, afanya hili kwa 2Face Idibia

Diamond Platnumz anaitumia vizuri ziara yake ya Ulaya. Akiwa jijini Paris, Ufaransa alitembelewa na msanii mkongwe wa Congo, Awilo Longomba ambaye kumbe ni rafiki yake wa muda mrefu na Zari anayelielezea kutano lao kwa maneno ‘My good friend @awilolongomba came to visit, hope you do some business with hubby. Was great seeing you.’

12905229_1535891503380571_877978790_n

Hajaishia hapo – ameingia studio na Fally Ipupa aliyeiwekea maneno picha aliyoweka Instagram, ‘Music doesn’t sleep…with my Brother @diamondplatnumz.”
Kwa wasanii dakika chache za kukutana studio kinaweza kuzalisha hit kubwa.

12383347_1004171386303928_1152208413_n

Kupitia Instagram, Diamond ameielezea collabo hiyo: Natamani walau mngepata japo sekunde moja tu ya Kuskia tulichokifanya jana katika Ngoma Mpya alonishirikisha @fallyipupa01 ….. Mwenyewe anasema kabla ya Kushoot Video lazma tuiingilie Chimbo kama Wiki nzima Hivi na Madancers wetu wote, Full Dance na Mapande ya ajabu!

Katika hatua nyingine Diamond amewahi kuonekana akiimba wimbo wa 2face Idibia, African Queen mara kibao.

https://www.youtube.com/watch?v=brinr6KFmxU

Aliwahi kuuimba pia kwenye msimu wa pili wa Coke Studio Africa na kwa namna anavyouimba ni rahisi kugundua kuwa Mnigeria huyo amemuinspire kwa kiasi kikubwa.

Hivyo muimbaji huyo wa ‘Utanipenda’ ameamua kumpa heshima msanii huyo anayejiita 2 Baba kwa sasa kwa kuweka picha yake kwenye profile yake Instagram yenye followers zaidi ya milioni mbili sasa.

2 Face

Ni njia nzuri ya kutoa heshima kwa wakongwe na hiyo inamweka karibu nao – strategy!

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents