BurudaniDiamond Platnumz

Diamond na Wizkid kutumbuiza jukwaa moja kwenye tuzo za MTV Africa ‘MAMA’ Afrika Kusini wiki ijayo

Orodha ya wasanii watakaopanda jukwaani kutoa burudani katika tuzo za MTV Africa Music Awards (MAMA) inazidi kuongezeka, sasa MTV Base imewataja ‘Number One’ hit maker Diamond Platnumz, Wizkid na Phyno wa Nigeria pamoja na Yuri Da Cunha wa Angola kuwa miongoni mwa wasanii watakaotumbuiza.

Diamond (2)

Diamond ambaye pia anawania tuzo mbili za ‘Best Collabo’ pamoja na ya ‘Best Male’ katika tuzo hizo, anaungana na wasanii wengine wa Afrika kama Davido, Flavour, Tiwa Savage, Mafikizolo, Uhuru na Oskido ambao walikuwa wameshatajwa kutumbuiza.

Wizkid-pic
Wizkid

Wasanii wa kimataifa walioishatajwa kuperform siku hiyo ni pamoja na mwimbaji wa R&B Trey Songz, French Montana na Miguel. Host wa show hiyo atakuwa mchekeshaji na muigizaji wa filamu Marlon Wayans.

Tuzo hizo zitafanyika wiki ijayo (June 7) katika ukumbi wa ICC huko Durban, Afrika Kusini na zitaoneshwa live kupitia MTV, MTV Base, BET International na vituo vingine washirika.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents