Burudani

Diva apanga kuwashirikisha Iyanya, Tekno na Seyi Sheyi kwenye album yake, ‘The Life Of The Diva’

Mtangazaji wa Clouds FM, Diva amesema anaandaa album yake ya kwanza, ‘The Life Of The Diva’ itakayowashirikisha wasanii wa ndani na nje.

12816838_940079149440464_29362330_n

Ameimbia Bongo5 kuwa kwenye album hiyo anapanga kuwashirikisha wasanii wa Nigeria, Iyanya, Tekno na Seyi Sheyi. Wengine watakaokuwemo kwenye album hiyo ni Diamond, Ommy Dimpoz, Mr Blue na wengine na itakuwa na nyimbo 10 huku ikipatikana iTunes.

“Album itakuwa na wimbo wa Piga Simu feat Diamond, honored kufanya kazi na Diamond, forever thankful yaani he is such a good human being, no one is perfect, am not perfect pia but kiukweli wasanii wa Tanzania wana kila njia ya kujifunza toka kwake, he is such a good hearted, very supportive and alinisaidia sana katika Piga Simu,” amesema Diva.

“Ommy dimpoz yupo , mgonjwa kwa raha zako Mr. Blue yumo as well , then Jicho la Huba, Stereo and Gosby, Nina Mashaallah as well na Bob Junior and nina nyimbo ambazo Chidi Benz atashiriki kuandika ambazo ndio zita lead kwenye album yangu,” ameongeza.

Kwa upande mwingine, Diva ameshikishwa na Chege kwenye wimbo wake mpya Champagne utakaokuwepo kwenye album yake.

“Chege ni mmoja kati ya watu wenye melody za haraka and very catchy learned a lot , and pleasure kuwa na studio session naye. It was unplanned though, was there with Mr. Blue for my song and Vhege was there so tukafanya tulichofanya and Dunga Mandugu Digital and Lamar was there, so everything was dope.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents