Habari

Dj Majay leo kuzindua upigaji muziki akiwa na mpiga drums ‘Live Dj With the Drum Music’ Maisha Club

Xtreme Deejayz leo wanazindua upigaji mpya wa muziki kwenye club ambapo DJ Majay atakuwa akipiga muziki New Club Maisha akishirikiana na mpiga drums.

Majay final 02

“Dj kama dj anaplay as a Dj na drummer anajazia flava zake,” Majay ameiambia Bongo5.
_DSC0882 copy_1
Dj Majay

“Sio lazima (drummer) afuatilizie kinachopigwa anaweza akawa anapiga kitu ambacho hakipo katika wimbo kama kucreate new flava,” amesema Majay.

Majay amesema yeye na mpiga drum huyo wamefanya mazoezi ya kutosha na watakuwa wakicheza nyimbo za aina zote. Amesema mpiga drum atakayekuwa naye anaitwa Harry aka Zungu.

DU7C6191

“Ni kijana tu Mbongo ambaye ana experience na mambo ya drums, tukamchukua tukamwelekeza tunachotaka kumtoa katika ile perception ya kibendibendi na kumweka katika sura ya kidisco,” Majay amemuelezea Zungu.

Amesema watu watakaokuwa wakicheza watapata burudani zaidi kuliko upigaji disco wa kawaida na kumuona mchezaji drum pamoja na DJ huyo live wakifanya mambo yao.

Majay amesema kitu kilichomsukuma kuanzisha utaratibu huo ni hamu ya kuwa na extended version ya nyimbo kali duniani na kuzitengeneza ladha tofauti ya club.

Msikilize zaidi hapa.

[soundcloud url=”http://api.soundcloud.com/tracks/114841179″ params=”” width=” 100%” height=”166″ iframe=”true” /]

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents