Burudani

Ebitoke adai ‘kiss’ la kwanza la Ben Pol lilimchanganya

Mchekeshaji kutoka Timamu Media, Ebitoke ambaye kwa sasa anadaiwa kuwa mapenzini na Rnb Super Star Bongo, Ben Pol ameelezea moment aliyokutanayo  siku ya kwanza muimbaji huyo alipomkiss.

“Unajua mtu unayempenda halafu akikukiss lazima mwili usisimke kwanza, yeah mimi nilisisimka, nilisema mama!!!, nilihisi kama nipo mbinguni,” amesema Ebitoke.

Katika mahojiano na EATV alipoulizwa ex boy friend wake anachukuliaje drama zinazoelndelea kati yake na Ben Pol, mchekesaji huyo aliendelea kushikilia msimamo wake kuwa hajahi kuwa na mtu.

“Sina boy friend na sijawahi kudate na mtu, Ben ndio wangu wa kwanza,” alisisitiza.

By Peter Akaro

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents