Bongo5 Exclusives

Exclusive: Kinara wa Antivirus amtukana Cyrill kwa kuvumbua slogan ya Fiesta ‘Bhaasss”, Cyrill ajibu!!

Cyrill aka Kamikaze (Kulia)

Katika muda ambao kila mmoja anaamini kuwa nguvu ya Anti Virus ilishakufa siku nyingi baada ya kiongozi wake mbunge wa Mbeya Mhe. Joseph Mbilinyi kusuluhisha uadui wake na Ruge Mutahaba wa Clouds FM mapema mwaka huu, kinara mwingine wa kundi hilo ajulikanaye kwa jina la Peenlawyer amemshambulia rapper Cyrill kwa kuzalisha msemo wa Fiesta 2012, ‘Bhaasss’.

Kupitia Facebook Peenlawyer ameandika:

“Kama Cyrill ndie aliyependekeza neno BHaaasss la fiesta, BASI K****a yake..na akae akijua mambo BHAAADO sana!!na hizi si taarabu zenye vijembe,kama vivyo vya ooh sijui BHasssi,haya ni maisha na uwazi,tena haswa kwa ma rapper eti BHAas? Cyrill jiulize ni wakongwe wangapi walishauka kama wewe na ubishoo wakujidai na hao watoto wa dawasco(wafu),, kumbuka kulikuwa na wakongwe waliokuwa wakijishau kama wewe na kujipendekeza kwa hao jamaaa na mwisho wa siku wanakutumia kama kondom,kujikinga na magonjwa kama gono na wakimaliza watakumwaga kama MB DOG,Mr Nice,Maze B, Ray Cc nk,na utabaki na gono lako koz we ni condom tu, tena K**a la mama yako kila nikisIkia hilo neno mtaani,unaona furahi kubang kwenye empire ya kibepali,mwanao atakuja kukudai kwa u***ge unaomuwekea kwenye history ya muziki! Uwazi mixtape ndio iko mtaani na ina majibu yako!Go n get it.”

Peenlawyer

Kufuatia shambulio hilo la makusudi kwa Cyrill Kamikaze, Bongo5 imeongea naye asubuhi ya leo na kuelezea jinsi alivyojisikia:

“Hiyo Bhasss ni neno ambalo lilikuwepo way back, yeye anaandika vitu ambavyo hajui . Basi ni neno ambalo tulikuwa tunalitumia mimi na kundi langu sasa wao ni watu ambao kila siku tumekuwa tukiroll now, kwahiyo wamelipenda wakaamua kulitumia. Hizo personal issues zao wasilete kabisa. Wao kama wana imani muziki wanataka kuupeleka mbali wasilete personal issues zao kwa mtu mmoja mmoja kwani ni radio moja tu ambayo haipigi nyimbo zao? Kila inapofika Fiesta kila inapofika nini, kwahiyo hawa ni watu ambao wanakuwa wanatamani kupata kitu fulani wanashindwa, lakini what is supposed to be ni kutengeneza muziki mzuri tu, hakuna mtu anawabania, na kama ni strategy wewe unaweza ukaona, anasema mtu mmoja ndio anashikilia muziki lakini sio kweli unajua, mwisho wa siku wale ni wafanyabiashara tu na wenyewe.

Kwanini wasitafute njia kama wale wafanyabiashara wanadai wananyonya wasanii, kwanini wasitafute njia nyingine? Sio kutengeneza mixtape na kutukana mtu mmoja, ni kwasababu wao wana akili finyu na upeo wao ni mdogo sana. Yaani mimi kwanza nilihisi hili group lingefika mbali lakini nilishalitoa kabisa akilini na nikaona ni wapuuzi way back.

Kwahiyo wao leo hii kunitukana mimi matusi kama haya sishangai sababu nilishajua ni watu wenye ‘inferiority complex’ na wana ‘stress za muziki’ that’s all.

Tulipomuuliza kama anamfahamu Peenlawyer Cyril amesema, “Simfahamu na wala simjui na sitaki kumjua, yeye namchukulia ni bishoo tu, amenichukulia kibishoo na kunitukania mama yangu, ni ktu ambacho mimi kimenikera. Kama kweli we ni mwanaharakati si mtu wa kumtukania mtu mama yake, una create nini kwa watu ambao wanakuangalia na watu wengine wanasupport!! Kwahiyo hicho ni kitu ambacho mimi naona ni kitu ambacho hakina sense na watu wanaofanya wote hawana akili vizuri.

Yaani siko meza nao moja na sitakuwa meza nao moja, maisha. Wao wamefeli, wamefeli strategy zao kwasababu walikuwa wanamsupport mtu mmoja ambaye mtu huyo mmoja walisahau kuwa ana personal interests na sio kuukomboa muziki, wanajua wenyewe kilichotokea. Na huyo Peen asinijaribu wka style yoyote kwasababu sisi tunaishi Tanzania halafu tunapita kwenye mitaa hivi hivi.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents