Habari

Exclusive: Madee kuja na movie ya ‘Nani Kamwaga Pombe Yangu’

Mwanamuziki wa kundi la Tip Top Connection anayetamba na ngoma yake ‘Sio Mimi’, Madee amesema kwasasa anaendelea na project ya kuandaa movie yenye jina hilo ikiwa ni mwendelezo wa wimbo wake huo.

IMG_0301

Katika movie hiyo Madee atakuwa mwigizaji mkuu na atamshirikisha mwigizaji na mchekeshaji Zimwi pamoja na waigizaji wengine.

Akiongea na Bongo5, Madee alisema, “kuna comedian movies inakuja inaitwa “Nani Kamwaga Pombe Yangu” ambayo itachezwa na mimi mwenyewe, kuna Zimwi watu ambao wana deal na hivi vitu ndio nitajoin, baada ya miezi miwili au mitatu nitaongea zaidi na zaidi kitu gani kinaendelea lakini hiyo movie ‘Nani Kamwaga Pombe Yangu’ inakuja na tumeshaanza kushoot, nadhani baada ya wiki itakuuwa imeisha,ila baada ya miezi mitatu tutatoa taarifa kwenye vyombo vya habari.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents