Fahamu

Fahamu: Kisiwa chenye upungufu wa wanawake

Kisiwa cha Forea ndio kisiwa pekee kwa sasa duniani chenye upungufu wa wanawake. Kisiwa hicho kina idadi ya watu wapatao 50,000, kikiwa ni muunganiko wa miamba 18, vikiwemo visiwa vya volcano islands kati ya Iceland na Norway kwa upande wa Kaskazini mwa Bahari ya Atlantic.

Kuna takriban wanawake 300 kutoka nchi za Thailand na Ufilipino wanaoishi katika kisiwa cha Faroe. Katika miaka ya hivi karibuni visiwa vya Faroe vimepata upungugufu wa idadi ya watu huku vijana wengi wakiondoka kwenye kisiwa hicho kutafuta elimu na kutokurudi tena kuishi katika eneo hilo.

Waziri mkuu wa Forea Island, Axel Johannese ameeleza kuwa kisiwa hicho kina upungufu wa jinsia ya kike huku kukiwa na uchache wa takriban wanawake 2000 ikilinganishwa na wanaume.

Kutokana na upungufu huo, baadhi ya wanaume katika kisiwa wamelazimika kutumia mitandao ya mahusiano (dating sites) kutafuta wanawake kutoka maeneo mengine.

Idadi kubwa ya wanaume katika kisiwa hicho wamepata wake kupitia mitandao hiyo huku asilimia kubwa wakiwa wageni kutokea bara la Asia.

Na Laila Sued

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents