AfyaFahamu

Fahamu: Mmea wa Rosemary huimarisha kukumbuka

Watafiti nchini Uingereza wamesema huenda harufu ya mmea wa rosemary ikawa na uwezo wa kumsaidia binadamu kukumbuka mambo.

Mmea huyo, ambao huwa na maua ya rangi nyeupe, waridi, zambarau au samawati, sana hutumiwa kama kiungo kwenye chakula, vinywaji au mchuzi.

Utafiti umebaini kwamba wanafunzi waliokuwa kwenye chumba kilichopulizwa harufu ya rosemary, kwenye mfumo wa mafuta, walikuwa na uwezo wa kukumbuka mambo kwa asilimia 5 hadi 7 zaidi kuliko wanafunzi ambao hawakunusa harufu hiyo.

Mark Moss, kutoka Chuo Kikuu cha Northumbria anasema matokeo ya kutumia mmea huyo yalikuwa sawa pia kwa watu wazima.
Wanafunzi walioshirikishwa hawakuwa wanafahamu kwamba walikuwa wanachunguzwa kuhusu uwezo wa harufu hiyo, na tafiti imeonyesha kwamba waliokuwa katika vyumba vyenye harufu ya rosemary waliimarika kwenye matokeo yao ya kumbukumbu kwa zaidi 5% hadi 7%.

Dkt Moss alisema utafiti wake na Earle ulithibitisha kwamba mmea huo una faida kwa watoto na watu wazima. Lakini kuna tofauti katika kiwango cha manufaa kwa watu mbalimbali. Kuna baadhi ambao hawakufaidi kwa vyovyote vile katika uwezo wao wa kukumbuka mambo.

Dkt Moss anasema Rosemary una chembe za kusafirisha ujumbe wa neva katika ubongo ambazo huhusika katika kumbukumbu.

Chanzo BBC

Na Laila Sued

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents