Habari

Zimbabwe ni tajiri wa pili Afrika nzima -Mugabe

Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe amesema kuwa nchi yake ya Zimbabwe ndio taifa lililoendelea zaidi katika bara Afrika baada ya Afrika kusini.

‘Tuna takriban vyuo vikuu 14 na asilimia 90 ya watu wamekwenda shule, ikiwa ni kiwango kikubwa zaidi barani Afrika’ huku akiongezea kwamba uchumi wao unaendelea kuimarika.

Hata hivyo Rais Mugabe amekana madai kwamba taifa hilo lina hali tete.

Zimbabwe imekuwa ikishindwa kuwalipa wafanyikazi wa serikali na huku ikiwekwa katika nafasi ya 24 kulingana na ripoti ya shirika la umoja wa mataifa UNDP, ya maendeleo barani Afrika.

Na Laila Sued

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents