Burudani

Fid Q aahidi video kali baada ya kugundua kuwa udhaifu wake ni kuwa na video za kawaida

Rapper Fareed Kubanda aka Fid Q amesema ameangalia udhaifu alionao kwenye muziki wake na amegundua kuwa huwa hana video kali.

Fid q

Akiongea leo kwenye kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Radio, Fid amesema mashabiki wake wategemee video kali kutoka kwake ili kuuondoa udhaifu huo.

Katika hatua nyingine, Fid Q amesema amewainspire 95% ya rappers wa Tanzania ndio maana anajiamini.

“Katika hip hop kuna mambo mengi, kuna suala linaitwa industry impact, kazi zako zikoje tangu ‘Huyu na Yule’ akina Dot.com vitu vimeendelea, zimekuja Mwanza Mwanza, Binti Malkia, August 13 mpaka leo tupo katika ‘Siri ya Mchezo’,” amesema.

Fid ambaye mwaka huu ameshinda tuzo mbili za KTMA, amesema pia suala jingine ni uwezo wa kubadilika ‘versatility’ kwenye nyimbo zake.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents