Burudani

Finding Dory yavunja rekodi ya filamu za animation

Filamu ya animation, Finding Dory imeweka rekodi mpya kwa kuwa filamu ya aina hiyo iliyoingiza fedha nyingi katika wiki yake ya kwanza.

dory-list

Kwa mujibu wa The Hollywood Reporter, filamu hiyo imeingiza dola milioni 136.2 tangu itoke Alhamis iliyopita na kuivunja rekodi ya Shrek the Third, iliyoingiza $121.6m mwaka 2007.

Kwa ujumla imekamata nafasi ya 18 kwa filamu zote zilizofungua vizuri katika wikiendi ya kwanza.

Finding Dory ni muendelezo wa filamu ya mwaka 2003, Finding Nemo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents