Habari

Gavana aliyetusi Uislamu ahukumiwa kifungo

Basuki Tjahaja Purnama ama Ahok ndiye alikuwa Gavana wa jimbo la Jakarta na sasa ameondoka madarakani na atatarajiwa kutumikia kifungo cha miaka miwili jela.

Ahok anahukumiwa kifungo hicho kutokana na matamshi yake ya kutusi dini ya kiislam katika nchi ya Indonesia. Ahok ambaye ni mkristo wa kwanza aliyeteuliwa Kwenye nafasi ya meya wa Jakarta, Yongolo, alitumia moja ya mstari wa Quran katika kampeni zake na kupelekea kukufuru mstari huyo.

Hata hivyo Ahok amekana kukufuru mstari huo na amesema kuwa atakata rufaa mahakamani, Kesi hiyo ya Gavana ilikuwa kesi yenye uvumilivu kwa dini zote mahakamani. Matamshi ya Gavana huyo yaliweza kuchochea ghasia.

Kufuatia hali hiyo Ahok amehukumiwa kifungo cha miaka miwili jela. Kabla ya hukumu kutolewa waandamanaji waliomuunga mkono na wale waliokuwa wakimpinga walitaka aachiliwe huru huku wengine wakitaka afungwe jela kwa muda mrefu.

Takriban maafisa 15,000 wa usalama kutoka maafisa wa polisi na jeshi wanaweka usalama katika eneo hilo huku maafisa wa polisi wa kukabiliana na ghasia na magari ya kivita yakiyatawanya makundi hayo mawili.

Na Laila Sued

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents